- UTANGULIZI
Programu ya msaada wa elimu (Education Support ESP) ilianzishwa mwaka 1997 ndani ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote(EOTF), kwa lengo la kukidhi changamoto za elimu kwa watu maskini, wasiojiweza, walemavu, yatima na watoto wasio na makazi kupitia kuwasaidia karo za shule, kusaidia wanafunzi, taasisi na shule vifaa vya elimu na kusaidia ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule mbali mbali.
- KARO ZA SHULE
Tangu kuanza kwa programu hii, EOTF imefanikiwa kuwasomesha jumla ya wanafunzi 1755 kwa kulipa karo za shule katika ngazi mbali mbali za elimu kama ifuatavyo;
- Shule ya awali wanafunzi 32
- Msingi wanafunzi 200
- Sekondari wanafunzi 974
- Ufundi Stadi VETA 178
- Vyuo vikuu vya ndani 262
- Vyuo vikuu vya nje ya nchi 21
- Watoto wenye mahitaji maalum 88
(Orodha ya wanafunzi wote waliosomeshwa imeambatanishwa)
- UKARABATI NA UJENZI WA MADARASA
EOTF imesaidia kufanikisha ukarabati na ujezi wa vyumba 17 vya madarasa katika shule za Kibaha, na Dar es salaam ambazo ni;
- Shule ya awali Ilala Boma – Dar es salaam
- Shule ya awali Simbani – Kibaha
- Shule ya msingi Makongo – Dar es salaam
- Shule ya msingi Kizuiani – Dar es salaam
- Ukarabati Mtoni Deaconic Lutheran Center – Dar es salaam
- Hedaru Sekondari – ujenzi wa Bwalo la chakula – Same Kilimanjaro
- Ukarabati kituo cha watoto yatima Kurasini – Dar es salaam
- MSAADA WA MADAWATI NA VIFAA VYA MAABARA
EOTF katika jitihada zake za kuiunga mkono serikali katika kutekeleza sera yake ya elimu, ilifanikiwa kusaidia kutoa msaada wa madawati madawati 808 na meza 451 kwenda kwenye shule mbali mbali kama ifuatavyo;
- Shule ya msingi Mbagala madawati 500 na meza 401
- Shule ya msingi Mpakani madawati 258
- Nachingwea meza 50 na na viti 50
- Vifaa vya maabara shule ya sekondari Kibasila
- MSAADA WA COMPUTA
EOTF ilitoa computa 44 kwa wahiaji mbali mbali kama ifuatavyo
- Shule ya sekondari Benjamin William Mkapa 24
- JKT Mgulani compute 10
- Kibaha Children’s Village Centre computa 10
- MSAADA WA VITABU
EOTF imeweza kusambaza jumla ya vitabu makontena 24 sawa na vitabu mabox 13,440 vyenye thamani ya dola za kimarekani240,000sawa na pesa za Tanzania shilingi milioni miatano hamsini na mbili (552,000.000). Vitabu vilisambazwa karibu mikoa yote ya Tanzania pamoja na nchi jirani ya Kenya kama ifuatavyo;
- Dar es salaam
- Mtwara
- Morogoro
- Lindi
- Pwani
- Njombe
- Iringa
- Kagera
- Mbeya
- Kilimanjaro
- Rukwa
- Tabora
- Arusha
- Dodoma
- Tanga
- Singida
- Mwanza
- Unguja
- Pemba
- Shinnyanga
- Songea
- Ruvuma
- Manyara
- Kigoma
- Kenya Book Source Trust= (copy ya majina ya mikoa iliyosambaziwa vitabu imeambatanishwa)
- MATOKEO:
EOTF inajivunia kupitia utekelezaji wa programu hii tumeweza kufikia malengo yetu yaliyowekwa wakati wa kuanzishwa kwa programu hii, ambapo fedha ziliweza kutolewa kuasaidia kulipa karo za wanafunzi wapatao 1755, ujezi na ukarabati wa shule uliweza kufanyika na matokeo yake mazingira ya elimu rafiki kwa watoto kujifunzia yaliweza kupatikana na hivyo tukafanikiwa kuzalisha wataalam katika fani mbali mbali za;
- Udaktari
- Sheria
- Tehama
- Uongozi
- Maafisa ustawi/social workers
- Mainjinia wa ndege
- Marubani
- Ualimu
- Uandishi wa habari
- Uanajeshi
- Ujasiriamali
- Uongozi
- Uhasibu
- Wapishi wa kimataifa
- Wahudumu wa hotel NA Mafundi katika fani mbali mbali.


